Featured
Loading...

Taarifa ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu mpya wa TCRA

Ally Yahaya Simba
Ally Yahaya Simba

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania Kifungu cha 13 (1) amemteua Dkt. Ally Yahaya Simba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 6 Julai 2015. 

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Ally Yahaya Simba alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Imetolewa na:

Selina Lyimo
KAIMU KATIBU MKUU
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KWA HABARI MOTO MOTO ZA TOWN | Designed By Code Nirvana
Back To Top